1 Chronicles 1

Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Ibrahimu

(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)

Adamu Hadi Wana Wa Nuhu

1 aAdamu, Sethi, Enoshi, 2 bKenani, Mahalaleli, Yaredi, 3 cIdrisi, Methusela, Lameki, Nuhu.


4 dWana wa Nuhu walikuwa:
Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi


5 Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

6 Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

7 Wana wa Yavani walikuwa:
Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

Wana Wa Hamu


8 eWana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misri,
Yaani Misri.
Putu na Kanaani.

9 Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.

10 gKushi akamzaa
Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.

11 Misri akawazaa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
12 hWapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

13 Wana wa Kanaani walikuwa:
Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,
14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,
15Wahivi, Waariki, Wasini,
16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu


17 iWana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

18 Arfaksadi akamzaa Shela,
Shela akamzaa Eberi.

19 Eberi alipata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi,
Pelegi maana yake Mgawanyiko.
kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

20 Wana wa Yoktani walikuwa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21Hadoramu, Uzali, Dikla,
22Obali, Abimaeli, Sheba,
23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

24 kWana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
25 lEberi, Pelegi, Reu,
26Serugi, Nahori, Tera,
27 mTera akamzaa Abramu (yaani, Ibrahimu).

Jamaa Ya Ibrahimu


28 nIbrahimu alikuwa na wana wawili:
Isaka na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

(Mwanzo 25:12-16)


29 oHawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:
Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura


32 pWana waliozaliwa na Ketura suria wa Ibrahimu walikuwa:
Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
Wana wa Yokshani walikuwa:
Sheba na Dedani.

33 Wana wa Midiani walikuwa:
Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara


34 qIbrahimu alikuwa baba wa Isaka.
Wana wa Isaka walikuwa:
Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

(Mwanzo 36:1-19)


35 rWana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.

36 sWana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.

37 tWana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

(Mwanzo 36:20-30)


38 uWana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

39 vWana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

40 wWana wa Shobali walikuwa:
Alvani,
Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian.
Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana.

41 yMwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

42 Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

(Mwanzo 36:31-43)


43 zHawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45 aaYobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46 abHushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48 acSamla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ng’ambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50 adBaal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
51 aeNaye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi,
52Oholibama, Ela, Pinoni,
53Kenazi, Temani, Mibsari,
54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.
Copyright information for SwhKC